POLICE NIGERIA: DAVIDO HANA SHTAKA LA KUJIBU JUU YA KIFO CHA RAFIKI AKE TAGBO UMAIKE

POLICE NIGERIA: DAVIDO HANA SHTAKA LA KUJIBU JUU YA KIFO CHA RAFIKI AKE
TAGBO UMAIKE

Wakili wa Davido Bobo F Ajudua amethibitisha taarifa kutoka polisi kuwa mteja wake Davido hana shtaka la kujibu katika kesi ya kifo cha rafiki yake Tagbo Umeike.
Davido anasema kupitia Twitter “Asante kwa wote walionimbea katika wakati huu na asante kwa wale hata waliosahau kuniombea, tunamshukuru mungu kwa yote na sasa turudi kwenye muziki, pia nimesamehe blogs na vyombo vyote vya habari vilivyo sambaza habari zisizo kweli kuhusu mimi, tuwe bora, tumshukuru Mungu”

Kauli hii imeonyesha wazi kuwa Davido amewekwa pembeni na polisi katika uchunguzi wa kifo cha rafiki yake Tagbo Umeike baada ya kugundulika kuwa sababu ya kifo cha rafiki yake ilikuwa ‘Kukosekana Hewa’ na sio Sumu kweny Pombe aliyokunywa wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa katika mgahawa wa Shisha huko Lekki, mjini Lagos.
Davido alihusishwa na kifo cha Umeike kutokana na kauli na tuhuma zilizotolewa na mpenzi wake Caroline Danjuma.

No comments

Powered by Blogger.